Jamii ya kibiashara ya Albino iliyoko Dar es Salaam AED, imempongeza balozi wake Mbwana Samatta anayecheza kandanda ya kulipwa kwenye klabu ya soka ya KRC Genk ya Ubelgiji kwa kufunga bao dhidi ya timu ya Everton ya Uingereza.
Kwenye taarifa kwa niaba ya jamii hiyo, mwenyekiti wa AED Michael Lugendo alisema kwamba bao la Samatta limedhihirisha uhodari wake na talanta yake katika soka ambayo inailetea sifa taifa la Tanzania.
Lugendo alisema, jamii hiyo inamwombea Samatta aendelee kutamba katika soka huku akidokeza kuwa jamii hiyo inajivunia kuwa naye kama balozi na msemaji wake anaposakakata soka ya kulipwa barani Ulaya.
No comments:
Post a Comment