Timu hiyo ilikuwa imetoka kushiriki mchezo wa ligi kuu
Taarifa kutoka
Ghana zinasema kwamba pametokea ajali ya gari lililokuwa limebeba
miongoni mwa timu kongwe nchini humo Asante Kotoko.
Mlezi wa timu hiyo ni mfalme wa Ashanti.
Timu
hiyo ilikuwa inarejea katika mji wake ambao ni wa pili kwa ukubwa
nchini humo , Kumasi baada ya mchezo wa ligi kuu mjini Accra dhidi ya
Inter Allies FC.
![]() |
| Asante Kotoko ni miongoni mwa klabu zinazotoa upinzani mkubwa Afrika |
Ajali hiyo imetokea katika sehemu iitwayo Nkawkaw kilomita 150 kutoka mji mkuu wa Ghana, Accra.
Inasemekana kuwa baadhi ya wachezaji wameumia vibaya akiwemo pia kocha wa timu hiyo na pia kuna kifo cha mtu mmoja.


No comments:
Post a Comment