NA ALPHOSE KUSAGA ARUSHA
Kondoo 12 wamekutwa wamekufa wakiwa kwenye banda lao na wengine 2 hawajulikani walipo katika Kitongoji cha KIRANYI wilayani Arumeru mkoani Arusha.
Akieleza shuhuda wa tukio hilo ambaye ni jirani anayeishi hatua chache kutoka katika banda hilo Aliyejitambulisha kwa jina la riziki amesema kuwa alisikia kelele majira ya saa kumi alfajiri akamua kuamka kuchungulia akaona wanyama wadogo wadogo jamii ya mbwa waliokuwepo eneo hilo.
Riziki amesema kuwa alipoona wanyama hao akamua kuwarushia mawe lakini alikuwa na woga kwasababu alikuwa hajui kwamba ni mnyama gani ndipo wakakimbia kusikojulikana lakini lakini walibeba kondoo wawili wadogo.
Akizungumza diwani wa kata ya Kiranyi Bwana John Seneu amesema kuwa tukio hilo ni la Kutisha kwasababu Kondo hao wamekutwa wamevunjika shingo na kupasuliwa katika maeneo ya Tumbo jambo ambalo hawajatambua nini kilichoua kondoo hao.
Akizungumzia tukio hilo Bi Thadea Mollel ambaye ni Afisa wanyama pori wa halmashauri ya Arusha Amesema kuwa wao wamefika eneo hilo na kujionea lakini hawajaona Nyayo zilizoonyesha kuwa kulikuwa na wanyama hao lakini wanashirikiana na wananchi watabaini chanzo chake.
Amesema kiutaalamu wamebaini kuwa ni mnyama aina ya Chui aliyefanya tukio hilo lakini kwa kushirikian na wizara ya maliasili na utalii na kitengo cha wanyama pori ili kubaini huenda kuna watu wanaofuga Chui maeneo hayo.

No comments:
Post a Comment