Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan
amesema Taifa halipo tayari hata kidogo kupokea misaada kutoka kwa
wafadhili wenye masharti ambayo hayaendani na mila na desturi za
kitanzania.
Mhe
Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo baada ya kukutana na kufanya
mazungumzo na Rais Mstaafu wa Ireland Mary Robinson pamoja na
mwanzilishi wa Taasisi ya Graca Machel, Craca Machel pamoja na ujumbe
walioambatana nao Ikulu- Jijini Dar es Salaam.
"Kuna
baadhi ya wafadhili wanaisaidia serikali katika utekelezaji wa miradi
ya maendeleo na bajeti vizuri sana na bila masharti mabaya lakini kuna
baadhi ya wafadhili wanaonyesha wazi kuwa wanataka serikali ikubali
masharti yao ambayo yanaenda kinyume na maadili ya taifa kitu ambacho
hakiwezekani" amesema Mhe. Samia.
Pamoja
na hayo, Mhe Samia Suluhu amesema kuwa serikali imeongeza maradufu
bajeti yake kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018 katika sekta ya afya ili
kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya kwa viwango vinavyotakiwa
nchini.
Kwa
upande wake, Rais Mstaafu wa Ireland Mary Robinson pamoja na
mwanzilishi wa Taasisi ya Kimataifa ya Graca Machel, Craca Machel
wameipongeza serikali kwa jitihada inazozifanya katika uimarishaji wa
sekta ya afya nchini na wameahidi kuendelea kushirikiana na serikali
katika kuhakikisha huduma za afya nchini zinaendelea kuboreshwa
ipasavyo.
No comments:
Post a Comment