Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema(Bawacha), Halima Mdee amezitaka halmashauri zinazoongozwa na chama hicho kuhakikisha zinawasaidia waliopata mimba shuleni kuendelea na masomo. Mdee ameyasema hayo leo Jumatatu wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano wake aliofanyia makao makuu ya Chadema jijini hapa.
Amesema viongozi wa halmashauri hizo hawapaswi kuogopa kutimiza wajibu wao kutokana na kauli ya Rais John Magufuli ya kuzuia wanafunzi wanaopata mimba kutoendelea na masomo.
Alisema wenyeviti wa halmashauri zilizopo chini ya Chadema waonyeshe mfano kuwa Tanzania ni nchi inayoongozwa kwa misingi Katiba na sheria ikiwamo ya elimu ambapo pamoja na mambo mengine inaweka misingi ya kupata elimu na kutobaguliwa kwa kigezo chochote.
“Nafahamu Rais anachukia wanawake, ana mfumo dume hii imeonyesha kwenye uteuzi wake, ila sikujua kama anawachukia hadi wasichana yaani msichana akipata mimba shule ndoto zake zinazimwa, wengine walibakwa,”alisema Mdee
No comments:
Post a Comment