Kenya imewasihi wahadhiri na wafanyakazi wengine kwenye vyuo vikuu vya umma kuacha tishio lao la mgomo kutokana na kuchelewa kwa utekelezaji wa makubaliano ya nyongeza ya mshahara yaliyofikiwa mwezi Februari.
Kwenye taarifa yake Waziri wa Elimu wa Kenya Fred Matiang’i amewataka wahadhiri kuacha mgomo huo uliopangwa kuanza leo akisema tayari nusu ya pesa hizo ambazo ni dola milioni 47 zimeshatumwa kwenye benki mbalimbali kwa ajili ya vyuo vikuu 31 vya umma, na kusisitiza kuwa kiasi kilichobaki kitatoka kwenye mwaka wa fedha 2017/2018.
Wahadhiri waliipa serikali hadi Ijumaa usiku kutekeleza makubaliano yao, na na kama ikishindwa kufanya hivyo wangeanza mgomo wao leo. Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Elimu ya Chuo Kikuu Constantine Wesonga amesema mgomo wa muda mrefu hauepukiki kama serikali inashindwa kutekeleza ahadi yake ya kuboresha mishahara ya wafanyakazi kwenye taasisi za elimu ya juu.
No comments:
Post a Comment