LATEST NEWS

Monday, July 10, 2017

MWINGINE AJINYONGA ARUSHA

 SINTO FAHAMU YAWAKUMBA WAKAZI WA ARUSHA KWA MFULULIZO WA MATUKIO YA KUJINYONGA

Matukio ya watu kujinyonga katika Mkoa wa Arusha yameendelea kuongezeka jijijni Arusha ambapo ikiwa ni siku moja tokea mwananfunzi wa darasa la sita katika shule ya msingi Olosiva akutwe amefariki dunia mara baada ya kujinyonga,mtu mwingene mkazi wa kijiji cha olgolai wilani Arumeru amekutwa leo asubuhi amefariki dunia mara baada  ya kujinyonga juu ya mti uliopo nyumbani kwake.
Mtu aliyejulikana kwa jina la Loishiro Kirasian miaka kati ya 45 hadi 47 amekutwa amejinyonga na maasai shuka kwenye mti wa mrufurufu na chanzo cha kujinyonga bhado akijafaamika 
Jeshi la polisi mkoani arusha linafanya uchunguzi kuhusu tukio hilo

MWILI WA MAREHEMU UMEPELEKWA NA JESHI LA POLISI KATIKA CHUMBA CHA KUHIFADHIA MIILI MOCHWARI HOSPITALI YA MANT MERU.

MAREHEMU PIA ANADAIWA KUWA SIKU YA JUMAMOSI NDIYO ALIFANYA SHEREHE YA KUCHINJA DUME LA RIKA LA LANDIISI KWA MILA ZA KIMASAI .
 
TAZAMA PICHA MBALI MBALI YA TUKIO
Picha ya Nyangusi Ole Sang'ida
MAREHEMU AKIINGIZWA KWENYE GARI LA POLISI 
 

No comments:

Post a Comment

Adbox