Mwenyekiti
wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) , Dionis Malinzi, ambaye ni ndugu
na Rais wa Shirikisho la Soka Jamali Malinzi ametumbuliwa leo na Waziri
wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Mwakyembe
kufuatia agizo la Waziri Mkuu
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alimtaka Waziri Mwakyembe kupitia baraza hilo na kulitathimini hivyo baada ya kulipitia na kutathimini amesitisha uteuzi wa Mwenyekiti wa baraza hilo.
"Kwa
mamlaka niliyopewa na sheria ya BMT Na. 12 ya 1967, nimesitisha uteuzi
wa Mwenyekiti na wajumbe wote wa BMT" amesema Dkt.Harrison Mwakyembe
Kwa
mujibu wa Waziri Mwakyembe amesema kuwa Sekretarieti ya Baraza la
Michezo Tanzania litaendelea na kazi kwa kushirikiana na serikali wakati
mchakato wa kuteua mwenyekiti mpya wa baraza hilo ukiendelea.
No comments:
Post a Comment