LATEST NEWS

Wednesday, July 26, 2017

Nyota wa raga nchini Kenya auwawa kwa kupigwa risasi

Jamii ya raga nchini Kenya inaomboleza kifo cha mchezaji James Kilonzo aliyepigwa risasi siku ya Jumatatu usiku na washukiwa wa ujambazi kwenye mtaa wa Kasarani.

Kulingana na taarifa, Kilonzo alipigwa risasi alipokuwa akitoa fedha katika mashine ya ATM. Kilonzo mwenye umri wa miaka 28 alikimbizwa hospitalini lakini akatangazwa kufariki muda mfupi baadaye.

Timu aliyoichezea ya KCB RFC inasema kifo cha nyota huyo ni pigo kubwa kwa jamii ya raga nchini Kenya. Kilonzo alikuwa miongoni mwa wachezaji waliosafiri kuelekea Afrika kusini kwenye kambi ya siku kumi baada ya kushinda kombe la Enterprise na Kenya Cup mwezi Mei mwaka huu. Alitajwa kuwa mchezaji bora wa ziara hiyo.

No comments:

Post a Comment

Adbox