Mwanariadha mahiri kutoka Jamaica Usain Bolt anasema
wanariadha ambao wanatumia dawa za kusisimua misuli lazima waache tabia
hiyo kwani inahatarisha maisha yao na michezo kwa jumla. Bolt anadai
kuwa taaluma ya michezo kwa sasa inakabiliwa na tishio kubwa kutoka
matumizi ya dawa hizo.
Bolt anayepanga kukimbia mbio ya mwisho katika taaluma yake iliyojaa
mafanikio, anasema anahofu hatima ya riadha iwapo tabia hii itaruhusiwa
kuendelea. Anasema ni maombi yake makubwa kwamba wanariadha wenzake
watasaidia juhudi za kusaidia michezo kusonga mbele wala sio nyuma kwa
sababu ya kutumia njia haramu kujipatia umaarufu.
Bolt mwenye umri wa miaka 30 amekiri kuwa madai yaliyotolewa hivi
karibuni kwenye ripoti ya McLaren kuhusu matumizi ya madawa hizo kwa
msaada kutoka watu fulani nchini Russia ni la kuhuzunisha na imeiletea
taaluma hiyo sifa mbaya.

No comments:
Post a Comment