Usain Bolt ana kipaji na ana
ushawishi mkubwa miongoni mwa wanariadha kama Muhammed Ali alivyokuwa na
ushawishi miongoni mwa mabondia, alisema Lord Coe.
BIngwa huyo wa
mbio fupi ambaye ameshinda medali ya dhabau katika michezo ya olimpiki
mara nane anatarajiwa kustaafu baada ya mashindano ya ubingwa mjini
London, yalioanza siku ya Ijumaa.
Coe alimfananisha raia huyo wa jamaica na mmoja wapo wa wanamichezo mashauri duniani Muhammed Ali.
Ni bingwa wa mbio fupi duniani,alisema Coe ambaye ndio raisi wa shirikisho la wanariadha duniani IAAF.
Usain
Bolt ana kipaji.Siwezi kumfananisha na mwanamichezo mwengine yeyote
yule zaidi ya Muhammad Ali, ambaye amekuwa na ushaiwishi mkubwa nje na
ndani ya michezo.
Unaweza kuanzisha mjadala kuhusu ni nani
mchezaji bora wa soka duniani ama mchezaji wa tenisi bora, lakini hakuna
mjadala kuhusu Bolt katika mbio fupi.
Mwanariadha huyo wa Jamaica
alishinda mio za mita100, 200 na 4 by 100 katika michezo iliopita ya
Olimpiki mjini Beijing 2008, mjini London 2012 na mjini Rio 2016

No comments:
Post a Comment