Baada ya Neymar kuwakimbia na kwenda PSG sasa inasemekana
klabu ya Barcelona iko mbioni kukamilisha usajili wa Osmane Dembele
kutoka BvB Phellipe Coutinho anayetoka Liverpool.
Klabu ya Chelsea wanaonekana wako serious sana na ishu ya kumnunua
Oxlade Chamberlain, inasemekana mabingwa hao wa ligi ya Uingereza
wamejiandaa kutoa £25m kumnunua.
Baada ya usiku wa jana Real Madrid kumuanzisha Gareth Bale sasa kocha
wa Manchester United Jose Mourinho amekiri kwamba haiwezekani tena
kumnunua.
Klabu ya soka ya PSG inaonekana inataka kuonesha tena umwamba wake
katika matumizi ya pesa na safari hii wamepiga hodi Atletico Madrid
kumnunua mlinda lango Jan Oblak.
Klabu ya Chelsea imejiweka mkao wa kula baada ya kiungo wanayemtaka
toka Leicester City Drinking Water kusema kwamba anataka kuondoka katika
klabu hiyo.
Inaonekana ka vita ya United na Chelsea katika usajili imerudi upya
baada ya Chelsea nao kumtaka Serge Aurier ambaye hapo mwanzo Manchester
United walikuwa wakimtaka.
Wednesday, August 9, 2017
Coutinho kwenda Barca huku Chamberlain akienda Chelsea
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment