LATEST NEWS

Friday, August 11, 2017

MAGARI YALIYOTELEKEZWA BANDARINI YATAIFISHWA WATUHUMIWA WAHUKUMIWA.


Baadhi ya Magari ambayo yalitelekezwa katika bandari ya jiji la Dar es Salaam na baadae yalikutwa na Rais Magufuli kwenye makontena, alipofanya ziara bandarini.

WATUHUMIWA waliongiza magari wakidai ni Nguo wahukumiwa
Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu wafanyabiashara wawili kulipa faini
ya Sh milioni 100 au kufungwa jela miaka mitatu baada ya kukiri kuingiza
magari matatu nchini na kujifanya kuwa ni mitumba.

Kitendo hicho kiliisababishia serikali hasara ya Sh milioni 190.9.

Watuhumiwa
hao, ambao ni Sultan Ibrahim na Ramadhani Hamisi, Raia wa Uganda,
wamehukumiwa adhabu hiyo na Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha.

Akisoma
hukumu hiyo, Mkeha amesema, licha ya ushirikiano waliotoa washitakiwa
ikiwemo kuomba kutaifishwa kwa magari hayo, ni matakwa ya sheria kwamba
mali hizo zitaifishwe na kwamba inazingatia thamani ya magari hayo
ambayo yamevuka kodi iliyotakiwa kupata serikali.

Amesema,
kila mshtakiwa anatakiwa kulipa fidia ya milioni 50 au kwenda jela
miaka mitatu na magari yote yataifishwe ili iwe onyo kwa yoyote
mwingine mwenye nia ya kukwepa kodi kwa namna hiyo ya washtakiwa.

Kabla
ya kusomwa kwa adhabu hiyo, hakimu Mkeha aliuuliza upande wa mashtaka
kama walikuwa na lolote la kusema ambapo, Wakili wa Serikali
Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi ameiomba mahakama kutoa adhabu kwa
kuzingatia kifungu namba 203 (b) cha Sheria ya Ushuru wa Forodha ya
Afrika Mashariki ya mwaka 2004 ambayo inataka bidhaa walizokutwa nazo
watuhumiwa kutaifishwa.

Hata
hivyo, wakili wa utetezi, Jebra Kambore aliiomba mahakama kuwaonea
huruma watuhumiwa hao kwani wametoa ushirikiano wa kutosha kwa kuandika
barua kwa serikali na kukubali magari hayo kutaifishwa.

Aliongeza, thamani ya magari hayo ni milioni 287,777,536 fedha ambazo ni zaidi ya kodi ambayo serikali ilitakiwa kupata.

Mapema
baada ya watuhumiwa hao kukiri mashtaka, walisomewa Maelezo ya awali
ambapo ilidaiwa, Desemba Mosi, 2016 na Machi mwaka huu, washitakiwa hao
na wengine wanaoishi Uingereza, walikubaliana kuingiza magari nchini.

Alidai
Oktoba 13, mwaka jana, kupitia nyaraka za kuingiza mizigo bandarini,
walishirikiana kuingiza kontena namba 3049836 ambayo ilibeba magari
matatu aina ya Range Rover Sports, Range Rover Evock na Range Rover
Vogue.

Aidha wanadiwa kutoa taarifa ya uongo
kupitia nyaraka hizo za kuingizia mizigo bandarini kwamba kontena hilo
lilibeba nguo za mitumba, viatu na magodoro kwa nia ya kukwepa kodi
ambayo thamani Mali hizo ilikuwa ndogo ukilinganisha na thamani halisi
ya magari waliyobeba.

Nyantori
alidai kutokana na uongo walioufanya, maofisa wa forodha wa Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) walikadiria kodi ya chini ya S milioni 31.5 badala
ya kodi sahihi iliyopaswa kul

Alieleza baadae, ilibainika kuwa kontena hilo lilibeba magari yaliyokuwa yamefichwa ndani ya mitumba ya viatu, magodoro na nguo.

‘’Mshitakiwa Sultan alipekuliwa nyumbani kwake na kukutwa na funguo tatu za magari hayo.

Awali
ilidaiwa, kati ya Desemba Mosi, mwaka jana na Machi 4, mwaka huu, Makao
Makuu ya Bandari wilayani Temeke, washitakiwa walitengeneza nyaraka za
uongo kuonesha kuwa kontena hilo lilikuwa na mitumba ambayo ni nguo,
viatu na magodoro na kuficha ndani yake magari hayo matatu.

Washitakiwa hao pia wanadaiwa kuficha utambuzi wa bidhaa waliyokuwa wakiingiza na kusababisha hasara ya Sh milioni 190.9.




Na Karama Kenyunko blogu ya jamii. 


No comments:

Post a Comment

Adbox