LATEST NEWS

Tuesday, August 22, 2017

TFF yamzuia Chirwa kuichezea Yanga dhidi ya Simba kesho

Image result for TFF 
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limemzuia kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mzambia Obrey Chirwa kucheza mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya mahasimu wao wa jadi, Simba SC mechi itakayopigwa uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kesho Jumatano. 

Ofisa habari wa TFF, Alfred Lucas katika mkutano na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam ameeleza kwamba, Chirwa hawezi kucheza kesho kwa sababu katika mchezo wa mwisho wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara dhidi ya Mbao FC alimsukuma refa mjini Mwanza.

No comments:

Post a Comment

Adbox