LATEST NEWS

Tuesday, August 15, 2017

Usain Bolt asema hatarudi nyuma baada ya kuamua kustaafu

Mwanariadha Usain Bolt amesema alitumia fursa ya mashindano ya ubingwa wa dunia yaliyomalizika jijini London Jumapili kama hafla ya kusema kwaheri kwa kila kitu alipokuwa akitia kikomo maisha yake kama mwanariadha.

Bolt, mwenye umri wa miaka 30, na ambaye pia ni mshindi wa dhahabu mara nane katika Olimpiki, amestaafu kutoka kwenye riadha baada ya kung'aa sana na kujizolea umaarufu si haba.

Lakini alipoulizwa iwapo atarejea kushindana tena, alijibu akisema amewaona watu wengi sana wakistaafu na kurudi tena halafu hali yao inakuwa mbaya zaidi au wanajiaibisha.

Raia huyo wa Jamaica anasema atakuwa mmoja wao. Hii ina maana kwamba bingwa huyo wa dunia mara 19, ambaye Lord Coe alimfananisha na Muhammad Ali, aliondoka kwa njia isiyo ya kawaida - akisaidiwa kuondoka uwanjani na wenzake, akiwa hawezi kusimama vyema wima baada ya kuumia.

No comments:

Post a Comment

Adbox