Wananchi jijini hapa wamekumbwa na hofu baada ya jana jioni kukutwa kwa miili katika eneo la ambayo iliibiwa hisia kuwa huenda ya watoto waliotekwa ambao walikuwa hawajapatikana.
Watoto hao; Moureen David (6) anayesoma darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Lucky Vincent na Ikram Salim (3), wakazi wa Kata ya Olasiti jijini Arusha wanadaiwa kutekwa huku polisi mkoani Geita wakimshikilia Samson Petro anayedaiwa kuwa mtuhumiwa mkuu .
Wakizungumza jana huku wakiwa wamekusanyika katika eneo la Olasiti Mtaa wa Olkerian katika Kata ya Olasiti; baadhi ya wananchi walisema kuwa wanasubiri taarifa ya polisi ambao ndio waliosimamia utoaji wa miili hiyo ili ifanyiwe uchunguzi na kubainika kuwa ni ya nani.
Awali , Mwenyekiti wa Mtaa wa Olkerian katika Kata ya Olasiti walikotekwa watoto hao, Daudi Safari amesema wana imani watoto hao watapatikana kutokana na kazi inayofanywa na polisi na wananchi.
No comments:
Post a Comment