LATEST NEWS

Wednesday, September 6, 2017

Mwili wa dereva wa bodaboda wazikwa mara ya pili



Baada ya mwili wa marehemu Juma Hamis(26), ambaye ni dereva wa bodaboda mkazi wa Bomambuzi kufukuliwa jana katika makaburi ya Pasua kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi kwa ajili ya kubaini chanzo cha kifo chake, mwili huo ulirudishwa kuzikwa tena katika makaburi saa 9 alasiri. Moshi.

Baada ya mwili wa marehemu Juma Hamis(26), ambaye ni dereva wa bodaboda mkazi wa Bomambuzi kufukuliwa jana katika makaburi ya Pasua kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi kwa ajili ya kubaini chanzo cha kifo chake, mwili huo ulirudishwa kuzikwa tena katika makaburi saa 9 alasiri.

Ndugu wa marehemu aliyeshuhudia kupasuliwa kwa mwili huo Salim Juma, amesema kwa mujibu wa daktari majibu yalionyesha kuwa alivunjika uti wa mgongo na kupata majeraha makubwa sehemu ya ubongo hali ambayo ilimsababishia mwili wake kupooza hadi umauti ulivyomkuta Julai 29 mwaka huu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamis Issah amesema tukio hilo ni la kiuchunguzi hivyo anasubiria majibu kwa maandishi kutoka kwa daktari aliyemfanyia postmoterm ili kuyakabidhi majibu hayo kwa wakili wa Serikali.

No comments:

Post a Comment

Adbox