LATEST NEWS

Friday, September 8, 2017

Lissu azinduka Nairobi

 
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji amesema kuwa mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho Tundu Lissu anaendelea vizuri na ameshazinduka.

Akizungumza na vyombo vya habari leo Ijumaa, Dk Mashinji amesema amezungumza na mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe ambaye aliongozana na Lissu kupata matibabu Nairobi nchini Kenya na amemueleza kuwa Lissu anaendelea vema na amezinduka baada ya dawa alizochomwa kwa ajili ya kupumzika na kusafiri kuisha.

Amesema damu ya Lissu imemwagika kabla ya wakati wake hivyo makamanda wa chama hicho nchi nzima waende kwenye hospitali na zahanati kutoa damu.

“Tuchangie damu kuhakikisha benki za damu zinakuwa na damu ya kutosha ili ziwasaidue wahitaji,” amesema Dk Mashinji. Dk Mashinji amesema tukio hilo halijawatisha badala yake limewaimarisha zaidi.

Alifafanua kuwa Lissu alimiminiwa risasi za kutosha kuashiria kulikuwa na lengo la kuua. Kwa upande wa Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Profess Abdallah Safari amesema wao kama wanasheria likitokea jambo kama lililomtokea Lissu huangalia mambo mawili makubwa, ambayo ni imetumika silaha gani na amepigwa eneo gani, hivyo kwa Lissu alilengwa kupigwa kichwa na kifua kuonyesha wazi kulikuwa na nia ya kuua.

#Mwananchi

No comments:

Post a Comment

Adbox