Wakongwe wa Manchester United wakiongozwa na Ruud van Nistelrooy wametoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya wale wa FC Barcelona waliokuwa wakiongozwa na Patrick Kluivert.
Hii ilikuwa ni mechi ya pili baada ya ile ya kwanza kwenye uwanja wa Camp Nou jijini Barcelona ambako wenyeji walipoteza kwa maba0 2-4.
Katika mechi hiyo kwenye Uwanja wa Old Trafford wenyeji ndiyo walianza kufunga mabao 2 hadi mapumziko.
Bao la kwanza liliwekwa kimiani na Van Nistelrooy kwa mkwaji wa penalti baada ya Karel Poborsky kuangushwa na Danny Webber akafunga la pili. Kipindi cha pili, FC Barcelona walisawazisha kupitia Luis Garcia na Gaizka Mandieta.
Monday, September 4, 2017
Manchester, Barcelona watoshana nguvu na kutoka sare
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment