KUUWAWA KWA MAJAMBAZI WAWILI NA KUPATIKANA KWA SILAHA AINA YA SMG RISASI KUMI NA TISA NA MAGANDA MAWILI
Jeshi
la Polisi Kanda Maalum Dsm mnamo tarehe 11.10.2017 majira ya saa nne
kamili usiku huko maeneo ya Mbezi Mshikamano kwa Mgalula, askari
walipata taarifa kutoka kwa FRANCIS MINDE miaka 30, mfanyabiashara
ambaye anamiliki duka la vitu mchanganyiko kwamba walifika watu wawili
katika duka lake wakitumia pikipiki aina ya Boxer nyeusi ambayo
haikusomeka namba na kumuuliza kama kuna huduma ya M-PESA na TIGO-PESA
na kuwajibu kuwa hakuna huduma hiyo, aliwatilia mashaka huenda sio watu
wazuri hatimaye alitoa taarifa Polisi.
Mara
baada ya kupata taarifa hizo askari walikwenda eneo hilo na kuiona
pikipiki ikiwa imeegeshwa gizani ikiwa na watu watatu, askari waliwaita
watu hao ili kuwahoji lakini watu hao walianza kukimbia huku wakifyatua
risasi upande waliopo askari, kuona hivyo askari nao walijibu
mashambulizi na kufanikiwa kuwajeruhi majambazi wawili, mmoja kati yao
alifanikiwa kukimbia na pikipiki waliyokuwa nayo
Aidha
eneo la tukio ilikutwa Silaha aina ya SMG yenye namba UC59821998 ikiwa
na magazine mbili, magazine moja ikiwa na risasi kumi na tisa (19) na
nyingine ikiwa tupu na maganda kumi na tatu (13) ya risasi aina ya SMG.
Katika
ufuatiliaji wa tukio hilo ilibainika kuwa mmoja wa majambazi hao
waliouwawa ni miongoni mwa watuhumiwa walioshiriki tukio la kuvamiwa kwa
Meja Generali mstaafu wa Jeshi la Wananchi VICENT KARIONGO lililotokea
mnamo tarehe 11/09/2017 majira ya saa kumi na moja jioni.
Majeruhi
wote wawili walifariki dunia wakiwa njiani kupelekwa Hospitali ya
Mwananyamala. Hakuna askari aliyeumia au kujeruhiwa, miili ya marehemu
imehifadhiwa Hospitali ya Mwananyamala. Jitihada za kumtafuta jambazi
aliyekimbia zinaendelea.
Wakati
huo huo, Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dsm mnamo tarehe 12.10.2017
majira ya saa nane na nusu usiku huko maeneo ya Mbezi Luis, Tegeta “A”
askari walipata taarifa kuwa katika Bar iitwayo TUMAINI, kuna majambazi
ambao idadi yao haijajulikana wakiwa na gari no. T 563 TAH aina ya
Toyota Noah rangi ya Blue ikiwa imetolewa viti vyote vya nyuma na kubaki
siti ya dereva na abiria, lengo lao lilikiwa ni kupakia vitu ambavyo
wangeiba kwenye Bar hiyo.
Wakati
wakiendelea na uvunjaji askari walifika eneo la tukio na baada ya
kugundua askari wamefika majambazi hao walifanikiwa kukimbia na
kutelekeza gari hilo, majambazi hao hawakufanikiwa kuchukua mali yeyote
na gari lipo kituo cha Polisi. Ufuatiliaji unaendelea wa kujua mmiliki
wa gari lililotumika katika tukio hilo.
POLISI
KANDA MAALUM DSM KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI KUANZIA TAREHE
06.10.2017 HADI TAREHE 11.10.2017 KIMEFANIKIWA KUKUSANYA TSH
466,350,000/= KWA TOZO ZA MAKOSA YA USALAMA BARABARANI
Jeshi
la Polisi kanda maalum Dar es salaam kupitia Kikosi chake cha Usalama
barabarani kinaendelea na oparesheni ya ukamataji wa makosa ya Usalama
Barabarani kwa kipindi cha kuanzia tarehe 06.10.2017 hadi tarehe
11.10.2017 kama ifuatavyo:-
- Idadi ya magari yaliyokamatwa – 14,340
- Idadi ya Pikipiki zilizokamatwa – 413
- Daladala zilizokamatwa -5,024
- Magari mengine (binafsi na malori) -1,205
- Bodaboda waliofikishwa Mahakamani kwa makosa ya kutovaa helmet na kupakia mishikaki -15
- Jumla ya Makosa yaliyokamatwa – 15,545
- Fedha za Tozo zilizopatikana – 466,350,000 /=
- Magari yaliyokamatwa kutokana na Kuchelewa kulipa faini kwa wakati – 2,832 (zaidi ya siku 7)
Kiasi kilicholipwa – 264, 673,4000/=
L .B.MAMBOSASA – SACP
KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM
No comments:
Post a Comment