Utafiti huo uliochapiswa katika jarida la New England Journal of Medicine, ulifanyiwa nchini Liberia na kuwashirikisha wagonjwa 1,500
Wale waliopewa chanjo hiyo walifanikiwa kupata kinga yenye nguvu kwa karibu mwaka mmoja.
Majaribio hayo yanaonyesha kuwa chanjo hizo zote zinaweza kutumiwa kuokoa maisha wakati wa majanga ya ugonjwa wa Ebola siku za usoni.
Ugonjwa wa Ebola uliwaua zaidi ya watu 11,000 nchini Liberia, Sierra Leone na Guinea, wakati wa mlipuko wa ugonjwa huo mwaka 2014-2015.
#BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment