LATEST NEWS

Wednesday, April 25, 2018

Binti wa Miaka 20 Amuua Mdogo Wake na Kumficha Uvunguni

 Binti wa miaka 20 ambaye jina lake halikutajwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi Temeke jijini Dar es salaam kwa tuhuma za kumuua mtoto wa miaka miwili, ambaye ametajwa ni mdogo wake na kisha kumficha uvunguni mwa kitanda huko nyumbani kwao Kigamboni jijini Dar es salaam.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Temeke Emmanuel Lukula amesema tukio hilo limetokea Jumatatu ya April 23, ambapo binti huyo alimchoma na kitu chenye ncha kali sehemu ya kitovu mtoto huyo na kumlaza kifudi fudi, kisha kutokomea kwa mpenzi wake.

“Ni kweli tukio hilo limetokea,aliyefanya hilo tukio ni binti wa miaka 20 ambaye ni ndugu wa mama wa marehemu, alimchoma huyo mtoto na kumlaza kifudifudi uvunguni kisha akaondoka kwa mwanaume anayedaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi, na baada ya mama wa mtoto kurudi kazini hakumkuta nyumbani”, amesema Kamanda Lukula.

Kamanda Lukula ameendelea kueleza kwamba baada ya hapo mama alitoa taarifa polisi, na baada ya uchunguzi walimkamata binti huyo na kuonyesha mahali alipomficha mtoto huyo, na mpaka sasa anashikiliwa jeshi la polisi ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa.

No comments:

Post a Comment

Adbox