LATEST NEWS

Monday, April 23, 2018

Watu 9 wauawa kwa kugongwa na gari la mizigo,Canada

Gari lililoua watu huko Canada
Watu tisa wameuawa mjini Toronto, nchini Canada baada kugongwa na gari la mizigo ambalo lilielekea katika mtaa wenye watu wengi. Wengine 16 wamejeruhiwa pia. Mashuhuda wanasema kuwa dereva huyo aliendelea kuliendesha gari takribani umbali wa kilomita moja hivi.

Diego de Matos yeye alikuwa akiendesha gari lake karibu na eneo hilo,amesema kuwa aliona watu wawili wakigongwa na gari hilo la mizigo.

"Lori hilo liliwagonga mwanamke na mwanaume.Hata hivyo baada ya kuwagonga watu hao dereva wa gari hilo aliendelea kuendesha gari hilo ambapo,mita chache mbele kulikuwa na miili mitano ama sita ikiwa chini.Na inavyoonekana dereva alikuwa akiyumbisha gari nje mara ndani ya mtaa huo,ilikuwa ni jambo la kutisha." Diego De Matos


Polisi mjini Toronto wakichunguza tukio la kuuawa kwa watu na Lori

Waziri wa usalama wa Canada Ralph Goodale amewaambia waandishi wa habari kwamba ni mapema kusema tukio hilo ni la kigaidi.

"Kuna ushirikiano wa kutosha kwa Polisi,katika kuchunguza jambo hilo,na tutatoa majibu ya hili kwa umma.Lakini kwa sasa hakuna taarifa zozote kwangu kuhusiana na chanzo ama lengo la tukio hili.'' Ralph Goodale

Kumekuwa na matukio ya magari makubwa kutumiwa na magaidi kusababisha vifo katika maeneo yenye mikusanyiko,baada ya mamlaka za usalama kudhibiti njia za magaidi hao zilizooeleka.

Matumizi ya magari makubwa ya mizigo,ni mfumo mpya ambao umekuwa ukitumiwa na magaidi kutekeleza azma yao kufuatia kubainika kwa njia zao zilizo mara zote.

No comments:

Post a Comment

Adbox