Friday, March 31, 2017

Sudan yapinga madai ya Umoja wa Mataifa kutaka Rais al-Bashir akabidhiwe kwa mahakama ya ICC

Serikali ya Sudan imepinga madai yaliyotolewa na naibu msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw Farhan Haq kutaka Rais Omar al-Bashir akabidhiwe kwa Mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai ICC.
Waziri wa mambo ya nje wa Sudan Bw. Ibrahim Ghandour amesema, serikali ya Sudan inatumai kuwa kauli ya msemaji huyo haiwakilishi msimamo wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Pia amesema serikali ya Sudan itafanya uchunguzi kwa njia ya kidiplomasia na kupitia ujumbe wake kwenye Umoja wa Mataifa, ili kujua chanzo cha taarifa hiyo, na inawakilisha mtu binafsi au Umoja wa Mataifa.

No comments:

Post a Comment

Adbox