
Mbunge wa Viti Maalumu kwa tiketi ya CHADEMA, Dokta Elly Macha ambaye alikuwa akiwakilisha watu wenye ulemavu amefariki dunia leo ijumaa ya Machi, 31 wakati akiwa katika matibabu nchini Uingereza.
Taarifa ya Bunge la Tanzania imeeleza kuwa Dk. Macha alikuwa amelezwa katika hospitali ya New Cross iliyopo mji wa Wolverhampton.
Taratibu za kuleta mwili wa marehemu tayari zimeanza kufanyika kwa bunge kushirikiana na ndugu wa marehemu ili kufanikisha mwili wa Dk. Macha kufika nchini na kuzikwa.
Aidha Spika wa Bunge, Job Ndugai ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu Dk. Macha pamoja na kuahirisha vikao vya kamati vilivyokuwa vikiendelea leo hadi kesho ya jumamosi ya Aprili mosi.
No comments:
Post a Comment