LATEST NEWS

Wednesday, April 12, 2017

Arsene Wenger aweka kitendawili kuhusu hatma yake na Arsenal

Mkufunzi mkuu wa timu ya Arsenal, Arsene Wenger, anasema kuwa hatma yake ya baadaye “haitawatatiza kwa vyovyote wachezaji.”
Aidha, Wenger anakiri kuwa mabao 3-0 waliyofungwa na timu ya Crystal Palace ni “jambo la kuleta wasiwasi mkubwa”.
Mkataba ya Wenger unamalizika mwishoni mwa msimu huu, huku akikabidhiwa mkataba mpya wa miaka mingine miwili, ingawa hajatangaza iwapo ataendelea kuifunza Arsenal au la. Arsenal iliyo katika nafasi ya 6, ina alama saba nyuma ya timu nne zilizoko katika nafasi za kwanza, huku ikisaliwa na mechi nane tu kukamilisha msimu huu.
Baada ya Arsenal kupata kichapo cha mbwa na timu ya Palace iliyo katika hatari ya kushushwa daraja, baadhi ya mashabiki wamemuambia Wenger, muda “umefika wa kuondoka”, huku pia wakiimba, “hufai kuvalia shati hilo”.
Kichapo hicho kinawaacha washikaji bunduki, katika hatari kubwa ya kukosa kufikia timu nne bora zitakazomaliza msimu huu, kwa mara ya kwanza katika historia ya miaka 67 iliyopita.

No comments:

Post a Comment

Adbox