Uongozi wa klabu ya Yanga umesema
umepeleka taarifa kwenye taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa
Takukuru na Jeshi la Polisi ili kufuatilia mwenendo wa utendaji kazi wa
kamati ya saa 72 ya TFF.
Mjumbe wa kamati tendaji ya Yanga, Salum Mkemi alisema wana
wasiwasi na kamati hiyo inaweza kuipa Simba pointi tatu kutokana wajumbe
wake wengi kuwa wanachama wa Simba.
Mkemi aliwataja wajumbe wa kamati hiyo Msafiri Mgoyi, Baruani
Muhuza na Boniface Wambura aliodai ni wanachama wa kugalagala wa Simba
hivyo uwepo wao katika kamati hiyo utaathiri maamuzi yatakayotolewa.
Hata hivyo, Ofisa Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara
alisema viongozi wa Yanga wanataka kuharibu mpira kwa kuingilia utendaji
wa kamati na Bodi ya Ligi.
Ofisa Habari na Mawasiliano wa (TFF) Alfred Lucas alizitaka pande
mbili kusubiri uamuzi utakaotolewa na kikao cha kamati kitakachoketi
leo.
Wednesday, April 12, 2017
Home
/
MICHEZO
/
Yanga yapeleka taarifa Takukuru na Polisi ili kufuatilia mwenendo wa utendaji kazi wa kamati ya saa 72 ya TFF
Yanga yapeleka taarifa Takukuru na Polisi ili kufuatilia mwenendo wa utendaji kazi wa kamati ya saa 72 ya TFF
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment