LATEST NEWS

Thursday, April 13, 2017

Wizi wa mbegu za zao la muhugo waathiri wakulima Pemba

WAKULIMA wa zao la muhogo wilaya ya Mkoani Pemba, wamelalamikia tabia iliojitokeza kwa kuibiwa mbegu zao za muhogo jambo ambalo likiwarejesha nyuma kimaendeleo.

Wakizungmza na mwandishi wa habari hizi kwa nyakati tofauti kufuatia mkulima mwenzao Mohamed Salim Juma wa Mtuhaliwa kung’olewa visiki vyake vya muhogo 200 alivyokuwa tayari ameshavipanda vipanda jambo ambalo liliwasikitisha wakulima hao.

Mkulima huyo alisema yeye juzi alipofika kwenye shamba lake, aligundua kung’olewa kwa mbegu zake 200 alizokwishazipanda bila ya kumjua aliyefanya tukio hilo.

Nae bibi Mwamini Haji Ussi wa Mkanyageni alisema, yeye aliibiwa mbegu zake alizotaka kuzipanda kisha watu hao wasiofahamika kung’oa na muhogo wake robo eka ambao ulikuwa tayari umeshastawi.

“Hata mie ni kweli juzi niliibiwa mbegu na muhogo kwenye shamba langu, maana kipindi hichi cha mvua, kila mmoja anataka kulima, ni kutokana na uhaba wa mbegu’’,alifafanua.

Kwa upande wake Kassim Bendera Vuia wa Mtambile, alisema alilazimika kutoa taarifa kituo cha Polisi Mtambile kufuatia kuibiwa mbegu zake zaote.

“Mimi niliibiwa mbegu tu, lakini muhogo wala haukung’olewa, na bahati nzuri, nilizikamata eneo la Jiondeni Mkoani, ingawa mwizi sikumjua’’,alinifahamisha.

Alifafanua kuwa, alipotaka taarifa za ndani juu ya wapi mbegu hizo mnunuaji huyo amezipata, alimueleza kuwa alinunua eneo la Mizingiani njia ya Wambaa, ingawa baada ya kufuatilia aligundua kuwa ndie aliefanya hivyo ni jirani yake.

Sheha wa shehia ya Mtambile Rajab Risasi, alisema hayajapokea taarifa zozote za wizi wa mbegu, na kuitaka jamii kuendelea kukinawirisha kikosi cha polisi jamii.

Katika wiki tatu sasa tokea kuanza kwa msimu huu wa mvua, kumekuwa kikiibuka malalamika kila siku, kutokana na wakulima wa zao la muhugo kuibiwa mbegu na muhogo. Na Haji Nassor Pemba

No comments:

Post a Comment

Adbox