Wabunge wawili wa CCM na Chadema wametaka Bunge liahirishne shughuli zake mara moja na kutoa nafasi kwa wabunge kujadili suala la utekwaji wa raia nchini.
Wabunge hao ni Hussein Bashe(Nzega Mjini) na Joseph Mbilinyi(Mbeya Mjini)wameomba mwongozo wa Spika kuhusu suala hilo leo asubuhi.
Bashe amesema ni muhimu suala hilo likajadiliwa kwani iko orodha ya wabunge 11 akiwemo yeye mwenyewe wameambiwa wakae chonjo.
Bashe alisimama kwa kutumia kanuni ya 47 vifungu (i,ii,iii) akamtaka Naibu Spika kusimamisha shughuli za bunge kwani jambo lililombele yao ni kubwa na likiachwa linaweza kuwa na madhara makubwa na kuichafua taswira nzima ya serikali.
Hoja ya mbunge huyo iliungwa mkono na Mbilinyi ambaye amesema kuwa Taifa limekuwa gizani kutokana na utamaduni wa utekaji ambao tangu mwanzo haukuwepo na akamtaka Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba kujihuzulu mara moja nafasi yake ili kulinda heshima.
No comments:
Post a Comment