Bw Tillerson anatarajiwa kuzuru Moscow baadaye wiki hii
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani, Rex Tillerson ameikosoa vikali Urusi, na kusema kuwa, ilishindwa kuzuia kutokea kwa shambulio la kemikali katika mji unaoshikiliwa na waasi nchini Syria.
Urusi ilikuwa imekiri awali kuhakikisha kuwa hifadhi ya silaha za sumu, imeharibiwa kabisa - na kwa kushindwa kufanya hivyo, kulichangia kutokea kwa shambulio hilo baya, alisema.
Mawaziri wa nchi za kigeni wa mataifa yenye nguvu za kiuchumi duniani- G7, wanajiandaa kukutana baadaye leo Jumatatu huko Italia.
Mazungumzo hayo yatalenga namna ya kuongeza shinikizo kwa Urusi kujitenga na Rais wa Syria Bashar Al-Assad
Mnamo siku ya Jumanne, Bw. Tillerson, ataendeleza mkutano huo wa G7 na kuwelekea Moscow, ambapo atakutana na waziri mwenzake wa mashauri ya nchi za kigeni wa Urusi, Sergei Lavrov.
Urusi ni mshirika wa karibu wa serikali ya Syria, na alisaidia kuwezesha muafaka wa mwaka 2013, wa kuharibu zana za sumu za Syria.
Shambulio lililoshukiwa kuwa la sumu, lilitokea mjini Khan Sheikhoun, Jumatano iliyopita na kusababisha vifo vya watu 89.Ili kujibu shambulio hilo, Marekani ilirusha makombora 59 yaliyolenga kambi za wanajeshi wa anga wa Syria.
Watoto walikuwa miongoni mwa waathiriwa wakuu katika shambulio hilo.
Syria imekanusha kutumia zana za sumu, huku Urusi ikisema kuwa Marekani haijatoa thibitisho lolote kuwa Syria ilitumia silaha za sumu katika shambulio hilo.
Source:Bbc Swahili
Monday, April 10, 2017
Marekani yailaumu Urusi kwa shambulio Syria
Tags
# KIMATAIFA
About Unknown
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
KIMATAIFA
Labels:
KIMATAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment