LATEST NEWS

Thursday, April 13, 2017

Gwajima afutiwa mashtaka ya kutoa lugha chafu


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeifuta kesi ya kutoa lugha chafu inayomkabili Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima.
Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha aliifuta kesi hiyo leo chini ya kifungu cha 225 cha sheria ya Mwenendo wa Makosa ya jinai (CPA).

Kesi hiyo imefutwa baada ya Wakili wa Serikali, Joseph Maugo kueleza kuwa hawakuwa na shaidi na kuomba wapewe ahirisho.

Katika kesi hii, Gwajima anadaiwa kuwa kati ya Machi 16 na 25,2015 Tanganyika Packers Kawe alitumia lugha chafu na kumdhihaki Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinal Pengo.

No comments:

Post a Comment

Adbox