LATEST NEWS

Thursday, April 13, 2017

Uelewa mdogo ni miongion mwa sababu zinazopelekea migogoro katika jamii



Uelewa mdogo wa jamii juu ya kumiliki Ardhi ni miongoni mwa matatizo yanayochangia kuengezeka kwa kesi za migogoro ya ardhi zinasababisha matukio mbali mbali ikiwemo kutengana kwa familia katika jamii.

Akizungumza  huko ofisini kwake vuga mjini Zanzibar mwanasheria kutoka mahakama ya Ardhi Muhsin Muhammed amesema kwa kipindi kirefu wamekuwa wakitowa elimu kuhusu umiliki wa ardhi lakini wengi wao wanajichukulia maamuzi yaliokinyume na sherika katika kumiliki ardhi.

Hata hivyo amesema kesi za migogoro ya ardhi zinazoripotiwa zimengezeka kwa kiasi kikubwa ambazo zinachangiwa na kuengezeka kwa maeneo ya uwekezaji pamoja na mipaka isifuata taratibu za kisheria.

Akizungumza maeneo yaliyokuwa na kesi nyingi za migogoro ya ardhi amesema ni pamoja na maeneo ya Wilaya ya Maghari hususan Magharib A ambapo maeneo hayo yamevamiwa na ujenzi holela usiozingatia sheria.

Amesema katika kipindi cha mwaka 2016 zaidi ya kesi mia mbili hamsini zimetolewa maamuzi hali inayoonesha kuengezeka kwa kesi hizo mahakamani hapo na kutowa wito kwa jamii kuwa kutumia vizuri elimu waliopewa pamoja na kuzitumia ipasavyo serikali za mitaa katika kusuluhisha kesi hizo.

Source:Zanzibar24

No comments:

Post a Comment

Adbox