NA CLEMENT SHARI - ARUSHA
Klabu ya soka ya Mtibwa Suger ya mkoani Morogoro imesema ipo tayari kuvaana na Stand United ya Shinyanga katika mfululizo ya michuano ya ligi kuu ya Vodacom mwishoni mwa wiki hii.
Msemaji wa Mtibwa Suger Thobias Kifaru Lugalambwike ameiambia Postline- Tz kuwa Timu yao ipo kamili kabisa kuchukua pointi zote tatu watakapokutana na Stand United siku ya Jumamosi huko mkoani Shinyanga na kwamba kikosi chao kipo kamili na hakuna majeruhi yeyote.
Mtibwa iliondoka Morogoro asubuhi ya Alhamisi hii kuelekea mkoani Shinyanga ikiwa na kumbukumbu nzuri ya mchezo wao wa mwisho ililazimishwa sare ya bila kufungana dhidi ya Azam Fc mchezo uliochezwa huko Manungu Turiani mkoani Morogoro.
Kifaru amekiri timu yao kufanya vibaya imetokana na shirikisho la soka nchini TFF kumchukua aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo Salum Mayanga ambaye kwa sasa ndiye kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars ambaye tangu kuondoka kwake timu hiyo imekuwa na mwenendo wa kusuasua katika ligi kuu ya Vodacom.
Thursday, April 13, 2017
Home
/
MICHEZO
/
Thobias Kifaru Lugalambwike: '"Tupo kamili kuchukua point 3 dhidi ya Stand United Jumamosi"
Thobias Kifaru Lugalambwike: '"Tupo kamili kuchukua point 3 dhidi ya Stand United Jumamosi"
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment