Klabu ya soka ya Jkt Ruvu imesema kwamba maandalizi yote
kuelekea pambano lao dhidi ya Azam fc litakalochezwa katika uwanja wa Mkwakwani
jijini Tanga siku ya Jumamosi yanaendelea vizuri.
Msemaji wa Jkt Ruvu Afisa mteule daraja la pili Constantine
Masanja ameiambia M-Media Tz maandalizi yote yapo vizuri na vijana wapo
tayari mkoani Tanga na wanachosubiria ni Jumamosi ifike wachukue pointi zote
tatu mbele ya Azam fc.
Masanja amewataka wakazi wa Tanga kujitokeza kwa wingi
katika uwanja wa Mkwakwani siku ya jumamosi na kuipa nguvu Jkt Ruvu ambayo
imeamua kuutumia uwanja wa Mkwakwani kama uwanja wake wa nyumbani kwa mechi
zote zilizosalia za ligi kuu ya Vodacom.
Jkt Ruvu ipo katika hatihati ya kushuka daraja kwani mpaka
hivi sasa ndio inayoshikilia mkia katika msimamo wa ligi kuu ya Vodacom na
iwapo itafungwa na Azam itakuwa inaashiria inaendelea kujichimbia kaburi
kuelekea ligi soka daraja la kwanza msimu ujao
No comments:
Post a Comment