LATEST NEWS

Saturday, April 15, 2017

Korea Kaskazini yaonya kuishambulia Marekani na makombora ya kinyuklia

Korea Kaskazini imeionya Marekani kutoanzisha vitendo vya uchokozi katika eneo la Korea ikisema kuwa iko tayari kulipiza kisasi kupitia mshambulio ya kinyuklia.

Taifa hilo limesema hivyo wakati ambapo kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un, amehudhuria gwaride la heshima katika mji mkuu wa Pyong yang, akiadhimisha siku ya kuzaliwa ya babu yake, marehemu Kim II-Sung, ambaye ni mwanzilishi wa taifa hilo.

"tumejiandaa kwa vita kamili'' ,alisema Choe Ryong-hae, anayeaminika kuwa mu wa pili mwenye uwezo mkubwa katika taifa hilo.''Tuko tayari kulipiza kisasi na mashambulio ya Nuklia kwa mbinu zetu dhidi ya shambulio lolote la Kinyuklia'' Jeshi la Korea Kaskazini likiwa katika gwaride la kijeshi

Huku kukiwa na wasiwasi kwamba Korea Kaskazini inakaribia kupata ufanisi wa kukamilisha silaha za Kinyuklia, Gwaride la Jumamosi ilikuwa fursa kwa bwana Kim kuonyesha uwezo wa kijeshi wa taifa hilo.

Vifaa vilivyoonyeshwa kwa mara ya kwanza vilikuwa vile vilivyotajwa kuwa manuwari za Pukkuksong ,makombora ya masafa marefu yanayoweza kwenda kwa takriban kilomita 1000.

Wachanganuzi wa vifaa vya kijeshi pia wanasema kuwa kuna makombora mawili mapya yanayoweza kurushwa kutoka bara moja hadi jingine, lakini haijulikani iwapo yamefanyiwa majaribio.

Kulikuwepo na sherehe za kawaida, kama vile mamia ya wanajeshi kupiga gwaride na msafara wa magari ya kivita huku yakiwa yamebeba silaha kama vile makombora
Maonyesha ya silaha nyingi yanaendelea nchini humo wakati ambapo kuna hali ya uhasama kati ya Korea Kaskazini na Marekani kufuatia mazoezi ya makombora ya kinyukilia yanayoandaliwa na Korea Kaskazini.

Hali ya wasiwasi imekumba eneo la Korea kwa ujumla kufuatia majaribio kadhaa ya makombora ya kisasa na Korea Kaskazini na mapema Jumamosi shirika la habari la taifa hilo lilionya Marekani kusitisha kiherehere chake cha vitisho vya kijeshi.


Marekani imetuma meli kadhaa za kivita katika Rasi ya Korea.


Hiyo jana waziri wa mashauri ya kigeni wa Uchina alionya kuwa vita vyovyote kati ya Korea Kaskazini na Marekani havitamfaidi ye yote.
BBC Swahili

No comments:

Post a Comment

Adbox