LATEST NEWS

Tuesday, April 4, 2017

Kamishna jenerali wa uhamiaji afanya mabadiliko makubwa ya viongozi wa mikoa nchini na baadhi ya viwanja vya ndege


                                  

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini Dr. Anna Peter Makakala amefanya mabadiliko makubwa ya Viongozi wa Uhamiaji wa Mikoa mbalimbali hapa nchini pamoja na kuwateua Wakuu Wapya wa mikoa kushika nyadhifa hizo katika Mikoa iliyopo Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar.

Katika Mabadiliko haya Naibu Kamishna wa Uhamiaji Sixstus Faustine Nyaki aliyekuwa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Mwanza amehamishiwa mkoa wa Simiyu wakati aliyekuwa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Rukwa Naibu Kamishna wa Uhamiaji Selemani Bandiho Kameya amehamishiwa Mkoa wa Tabora.

Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Mbeya, Naibu Kamishna wa Uhamiaji Asumsio Paulus Achacha amehamishiwa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Manyara Naibu Kamishna Peter Jerome Kundy amehamishiwa Mkoa wa Dodoma kuchukua nafasi ya Kamishna Msaidizi Ali Mohamed ambaye amehamishiwa kuwa Mkuu wa Uhamiaji mkoa wa Arusha.

Naibu Kamishna wa Uhamiaji Mkemi Mhina Seif ameteuliwa kuwa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Kusini Unguja, Naibu Kamishna wa Uhamiaji Muhsin Abdallah Muhsin ameteuliwa kuwa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini Unguja, Naibu Kamishna wa Uhamiaji Said Omary Hamdani ameteuliwa kuwa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Mjini Magharibi na Naibu Kamishna wa Uhamiaji Othman Khamis Salum ameteuliwa kuwa Mkuu wa Uhamiaji Mjini Magharibi Unguja.

Katika mabadiliko hayo baadhi ya Wakuu wa Uhamiaji wa Mikoa wamebaki katika Vituo vyao vya kazi vya awali akiwemo aliyekuwa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Morogoro Naibu Kamishna wa Uhamiaji Safina Muhindi, Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Lindi Naibu Kamishna wa Uhamiaji George Kombe, Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Ruvuma Naibu Kamishna
wa Uhamiaji Hilgaty Laurent Shauri, Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Singida Naibu Kamishna wa Uhamiaji Faith Alexander Ihano na Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Mara Naibu Kamishna Fredrick Eustace Kiondo.

Wengine waliobaki kwenye vituo vyao vya awali ni pamoja na Naibu Kamishna wa Uhamiaji Abdallah  Ramadhani Towo mkoa wa Kagera na Naibu Kamishna wa Uhamiaji Anastazia
Gasper Ngatunga mkoa wa Shinyanga.

Katika mabadiliko hayo Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dr. Makakala pia amewateua Viongozi wa Uhamiaji wa Mikoa wapya katika baadhi ya mikoa hapa nchini ambapo Naibu Kamishna wa Uhamiaji Mary Francis Palmer kuwa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Dar es
Salaam, Naibu Kamishna wa Uhamiaji Plasid Mazengo, Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Pwani, Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji James Andrew Mwanjotile, Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Mtwara,Kamishna Msaidizi Mwandamizi Hope Jaffer Kawawa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Iringa, na Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji Hosea Alphonce Kagimbo Mkoa wa Njombe.

Wengine ni Naibu Kamishna wa Uhamiaji Rashid Salum Magetta Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Songwe, Naibu Kamishna wa Uhamiaji Carlos John Haule, Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Rukwa, Naibu Kamishna wa Uhamiaji Julieth Deodatus Sagamiko Mkuu wa Uhamiaji Mkoa
wa Manyara, Naibu Kamishna wa Uhamiaji Albert Joseph Rwelamila, Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Kilimanjaro na Naibu Kamishna wa Uhamiaji Paul Laurent Eranga, Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Mwanza.

Naibu Kamishna wa Uhamiaji Crispin Crispin Ngonyani ameteuliwa kuwa Mkuu wa Uhamiaji
Mkoa wa Tanga, Naibu Kamishna wa Uhamiaji Shaban Omar Hatibu Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Katavi, Naibu Kamishna wa Uhamiaji Remigius Ibrahimu Pesambili Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Kigoma na Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji Novaita Edmund Mrosso ameteuliwa kuwa  Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Mbeya.

Aidha Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji Bakari Mohamed Ameir ameteuliwa kuwa Mkuu wa Kituo cha Uhamiaji cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume [AAKIA] na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhamiaji Fulgence Andrew Mutarasha kuwa Mkuu wa Uhamiaji Kituo cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere[JNIA].

                                             Imetolewa na  Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini
                                                                           Dr. A. P. Makakala
                                                                                3 Machi 2017


                                 

No comments:

Post a Comment

Adbox