Rais Vladmiri Putin wa Urusi akiweka maua kwenye eneo palipotokea mlipuko
Vikosi vya usalama nchini Urusi wako kwenye taadhari kubwa baada ya kutokea milipuko kwenye vituo viwili vya treni ya chini ya ardhi mjini St Petersburg.
Milipuko hiyo ilisababisha watu 11 kupoteza maisha na zaidi ya watu 40 walijeruhiwa.
Wachunguzi nchini Urusi wamelichukulia tukio hilo kuwa ni shambulio la kigaidi. Vyombo vya habari vimeripoti vikinukuu vyanzo vya usalama vikisema milipuko hiyo huenda imelipuliwa na mtu aliyejitoa muhanga kutoka eneo la Asia ya Kati.
Kifaa kingine kilichokutwa kwenye stesheni nyingine kiliteguliwa na wataalam wa kutegua mabomu.
Rais Vladmir Putin yuko St.Petersburg kupata maelezo ya wataalam wa masuala ya usalama, pia aliweka mashada ya maua kuwakumbuka walioathirika kwenye ajali hiyo, amesema ni mapema mno kujua chanzo cha tukio hilo lakini uchunguzi unafanyika.
''Sababu ya tukio hilo haijafahamika, hivyo ni mapema kuzungumzia kuhusu hilo.uchunguzi utaonyesha , lakini maelezo yote yatatizamwa, ilikupata sababu ya ajali hiyo na sababu ya uhalifu huo, juuu ya yote ugaidi, tutaona, uchunguzi utatupa majibu yote kuhusu kilichotokea.'' alieleza Putin
Source:Bbc Swahili
Tuesday, April 4, 2017
Aliyeshambulia Urusi anatoka Asia ya Kati
Tags
# KIMATAIFA
About Unknown
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
KIMATAIFA
Labels:
KIMATAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment