LATEST NEWS

Wednesday, April 19, 2017

Marekani: Korea Kaskazini ilikusudia kufanya uchokozi

Silaha Aprili 2017Marekani imesema Korea Kaskazini ilikuwa na nia fulani ilipotekeleza jaribio la kombora ambalo lilifeli mwishoni mwa wiki.
Waziri wa Ulinzi James Mattis amesema jaribio hilo lilikuwa la kutojali na kwamba Marekani "inafanya kazi kwa karibu" na China kukabiliana na Korea Kaskazini.

Amesema Korea Kaskazini ilifanya hivyo ikikusudia kufanya "uchokozi fulani".
Marekani ilisema kombora hilo la Korea Kaskazini lilipuka muda mfupi baada ya kurushwa angani.

Pyongyang imesema inaweza kuwa ikifanyia majaribio makombora kila wiki na pia ikaonya kwamba kutatokea "vita kamili" iwapo Marekani itaichukulia hatua za kijeshi.
 "Iwapo Marekani wanapanga kutushambulia, tutajibu kwa shambulio la nyuklia kwa mtindo na njia yetu wenyewe," naibu waziri wa mambo ya nje wa Korea Kaskazini Han Song-ryol aliambia BBC Jumatatu.

Pande zote mbili zimekuwa zikijibizana vikali baada ya Korea Kaskazini kufanya jaribio hilo la makombora.
Bw Mattis alisema kwamba jaribio hilo la Jumapili halikuhusisha kombora linaloweza kuruka kutoka bara moja hadi jingine lakini bado lilikuwa ishara ya kutojali.
"Inadhihirisha ni kwa nini tunafanya kazi kwa karibu kwa sasa na Wachina...tunajaribu kudhibiti hali hii na lengo letu ni kumaliza silaha za nyuklia katika rasi ya Korea," alisema.

Marekani inafanya nini?
Jumanne, taarifa kwenye gazeti la Guardian ilimnukuu afisa mmoja wa Marekani ambaye hakutajwa jina akisema Marekani inatafakari uwezekano wa kuyatungua makombora ya Korea Kaskazini yanaporushwa angani.
Marekani pia imetishia kukaza vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Korea kaskazini ambavyo vitahusisha marufuku ya kuiuzia mafuta nchi hiyo, marufuku kwa shirika la ndege la Korea Kaskazini pamoja na kusimamishwa na kupekuliwa kwa meli za Korea Kaskazini.
Aidha, vikwazo hivyo vitahusisha adhabu kali kwa benki za China zinazofanya biashara na taifa hilo, shirika la habari la Reuters limesema.
Hata hivyo, imebainika kwamba kundi la meli za kivita za Marekani, ikiwemo meli yenye uwezo wa kubeba ndege za kivita, hazikuwa zinaelekea upande wa Korea Kaskazini kama ilivyoripotiwa awali, bali zilikuwa zinaelekea eneo tofauti. Mike Pence
Kusini mwishoni mwa wiki. Hapa anaonekana akiangalia Korea Kaskazini kutoka eneo la Panmunjom mpakani .
 
Jeshi la wanamaji la Marekani lilikuwa limetangaza 8 Aprili kwamba kundi hilo la meli likiongozwa na meli kubwa ya Carl Vinson lilikuwa likielekea rasi ya Korea, kama hatua ya kuionya Korea Kaskazini.
Wiki iliyopita, Rais Trump pia alitangaza kwamba kundi kubwa la meli za kivita lilikuwa likitumwa eneo hilo.
Siku chache baadaye, Mattis alisema manowari hiyo ilikuwa "inaelekea huko".
Lakini imebainika kwamba ukweli ni kuwa meli hizo zilikuwa zinaelekea eneo tofauti.
Kufikia mwishoni mwa wiki, zilikuwa zimesafiri mbali sana na rasi ya Korea na zilikuwa zinapitia mlango wa bahari wa Sunda kuingia katika Bahari ya Hindi.

Korea Kaskazini inafanya nini

Korea Kaskazini imeongeza kasi katika majaribio yake ya makombora na silaha za nyuklia miaka ya karibuni licha ya marufuku ya Umoja wa Mataifa.
 
Naibu waziri wa ammbo ya nje wa nchi hiyo Han Song-ryol aliambia BBC kwamba Korea Kaskazini inaamini kwamba silaha zake za nyuklia zinaweza "kuilinda" dhidi ya tishio la shambulio la kijeshi kutoka kwa Marekani.
Korea Kaskazini inahofia kwamba Marekani na Korea Kusini wanaweza kutumia nguvu kumuondoa madarakani Kim Jong-un.

Katika Umoja wa Mataifa Jumatatu, mwakilishi wa kudumu wa taifa hilo katika umoja huo Kim In-ryong alishutumu mashambulio ya Marekani nchini Syria, ambayo yalilenga kambi ya ndege za kijeshi ya serikali ambayo ilituhumiwa kutumiwa kutekeleza shambulio la kutumia gesi ya sumu.Kim Jong-Un   
                  Kim Jong-un hajasafiri nje ya Korea Kaskazini tangu awe kiongozi wa nchi hiyo.
 
Alisema Marekani inatatiza amani na uthabiti duniani kwa kutumia fikira za kijambazi kuvamia mataifa huru.
Wachanganuzi wanasema Korea Kaskazini huenda ikafanya jaribio la sita la silaha za nyuklia hivi karibuni.Korea Kaskazini
  Uwezo wa makombora ya Korea Kaskazini
 
 
Source:BBC Swahili 

No comments:

Post a Comment

Adbox