LATEST NEWS

Monday, April 3, 2017

Polisi waua watatu Rufiji

 
Watu watatu ambao majina yao hayajatambulika wameuawa kwa kupigwa risasi na askari Polisi waliokuwa doria karibu na daraja la Mto Mkapa, wilayani hapa waakidhaniwa kuwa ni majambazi.

Akithibitisha kutokea kwa vifo hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani, Onesmo Lyanga alisema watu hao ambao wote ni wanaume walikuwa wameficha nyuso zao kwa hijabu na walikaidi agizo la polisi kila walipotakiwa kusimama.
 

Kamanda Lyanga alisema polisi walipewa taarifa toka kwa wasiri wao juu ya kuwepo kwa pikipiki tatu eneo la Kibiti, kwenye barabara ya Dar es Salaam kwenda Lindi zilizobeba abiria na pikipiki mbili kila moja ilikuwa imebeba abiria aliyefunika uso wake kwa hijabu.

Polisi waua watatu Rufiji Watu watatu ambao majina yao hayajatambulika wameuawa kwa kupigwa risasi na askari Polisi waliokuwa doria karibu na daraja la Mto Mkapa, wilayani hapa waakidhaniwa kuwa ni majambazi.
 

Amesema baada ya kupata taarifa hiyo Polisi waliwataarifu wenzao waliopo kwenye kizuizi cha Mparange ili wawasimamishe watu hao lakini watu hao baada ya kufika eneo hilo na kusimamishwa na Askari Polisi walikaidi kutii agizo hilo na kuendelea na safari yao wakiwa kasi.

No comments:

Post a Comment

Adbox