Na Senga Katoroki
Watu wawili wamefariki katika matukio mawili tofauti na
tukio la kwanza ni kifo cha kinyama cha mtu mmoja kukatwa shingo yake na
kitu chenye ncha kali yaani panga kisha kutumbukiziwa kitu chenye ncha
kali yaani kisu mdomoni mwake kisha kutokezea upande wa pili mwa shingo
yake huku mtu mmoja akifariki dunia kwa kupatwa na mshituko wa moyo
baada ya kwenda shambani mwake na kukuta majani yamezidi mazao hapa
wilayani babati mkoani manyara.
Katika tukio la kwanza mtu huyo alieuwawa mithili ya
nguruwe kwa kukatwa shingo yake kwa panga na kuchomwa kisu kikali
mdomoni mwake katika kijiji cha majengo kilichopo kata ya kashi wilayani
babati mkoani manyara ametambulika kwa majina ya hamis hasan nyalu.
Mashuuda wa tukio hili la kusikitisha akiwemo mjomba wake
marehemu hasan fautine na dada yake marehem Mariam Hasan wamethibitisha
ndugu yao kuuwawa kikatili.
baada ya hapo nimemtafuta diwani wa kata hio ya kashi John
kanda kwa njia ya simu kutokana na kutokuwepo ofisini kwake kikazi na
amethibitisha mtu huyo kuwawa ambaye ni mkazi wa eneo lake na alikua
akiishi mpakani mwa mkoa wa Manyara na Dodoma majengo.
kwa upande mwingine nilimtafuta kamanda wa jeshi la polis
mkoa wa manyara kamanda Francis Masawe ambapo amesema kuwa tayari
maafisa wa jeshi la polisi wamekwishafika fika eneo la tukio na kuchukua
mwili wa marehem huyo na kuupeleka katika zahanati ya galapo wilayani
babati mkoani hapa kwa uchunguzi.
na katika tukio la pili ambalo limetokea katika hospitali
ya wilaya ya babati mrara ni kua mtu huyo ambaye amefariki dunia
ametambulika kwa majina ya peter sebasitian ambaye aliwahi kuwa afisa
elimu wa wilaya ya Babati mkoani Manyara.
Wakiongea na mwandishi wa habari hizi ndugu na jamaa
wamesema kuwa afisa elimu huyo mstaafu alipatwa na mshituko na kuanguka
shambani kwake katika kijiji cha Gerimala baada ya kukuta shamba lake
lenye mazo likiwa halijafanyiwa palizi ili hali amekwishalipa pesa ya
kufanya palizi shamabini mwake.
alikimbizwa katika zahanati mbalimbali na vituo mbalimbali
hapa wilayani Babati lakini hali yake ilizidi kuwa mbaya na baadae
madaktari katika vituo hivyo vya afya walimwamru apelekwe katika
hospitali ya wilaya ya Babati Mrara.
Nao madakiri wa hospital hio walifanya kila jitihada wakati
huo akiwa katika chumba cha uangalizi maalum ICU na baadae madaktari
hao walithibitisha mtu huyo kuiaga dunia.
No comments:
Post a Comment