Takriban watu 10 wameuawa kufuatia milipuko iliyotokea kwenye vituo viwili vya treni ya chini ya ardhi mjini St Petersburg nchini Urusi.
Mashirika ya habari yanaripoti kuwa milipuko hiyo ilitokea kituo vya Sennaya Ploschad na kingine kilicho karibu cha Tekhnologichesky Institut, kati kati mwa mji.
Picha zilizowekwa kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha behewa kati kituo cha Sennaya likiwa limebaribiwa na watu waliouawa wakiwa karibu.
Rais wa Urusi Vladimir Putin anasema uchunguzi unafanywa.
Vituo vya habari vya Interfax na RIA viliripoti kuwa takriban watu 50 walijeruhiwa.
Rais Putin alikuwa mjini St Petersburg mapema Jumatatu lakinia kwa sasa hayuko mjini humo, kwa mjibu wa msemaji wake.
Mfumo wote wa usafiri wa treni ya chini ya ardhi mjini humo kwa sasa umefungwa na maasfisa wa usafiri wanasema kuwa wamengeza huduma za usalama.Mwaka 2009 mlipuko ulitokea kwenye treni moja ya mwendo wa kasi kati ya miji ya Moscow na St Petersburg, ambapo 27 waliuawa na wengine 130 kujeruhiwa
Source:Bbc Swahili
No comments:
Post a Comment