Waandishi wa Habari 66 kutoka Vyombo mbalimbali vya Habari Jumamosi ya Aprili 29, 2017 wanatarajia kuchuana vikali katika shindano la kuwania Tuzo ya Umahiri katika tasnia hiyo.
Waandishi hao ni kutoka vituo vya Redio, Runinga (Television) na Magazeti ambao hapo awali walikua 810, ambapo pia walichujwa na kufikia 66. Kati yao wateule 36 kutoka kwenye Magazeti, 16 Redio na 14 Runinga, wakati kati yao 20 ni Wanawake, 9 wanatoka kwenye Magazeti, 14 kwenye Runinga (TV).
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandali ya Tuzo hizo (EJAT), Kajubi Mukajanga amesema kuwa kwa muda wa wiki moja katikati ya Mwezi kati ya tarehe 6 – 13 Aprili, 2017, Majaji nane wamekuwa wakipitia kazi za Waandishi hao na baadaye kutambua zenye ubora.
Amesema kuwa idadi imeshuka kulingana na Mwaka uliopita kutokana na Mwaka uliopita idadi yao walikua Waandishi 84 waliofuzu kwa ubora wa kazi zao.
Kajubi amesema kuwa maoni ya Majaji kulikua na hamasa kubwa ya kuleta kazi lakini amesema kuwa nyingi hazikufikia vigezo, na hivyo kupelekea ugumu kuchagua wateule.
Katika zoezi hilo jopo la Majaji liliongozwa na Jaji Valerie Msoka, Ndimara Tegambwage, Hassan Mhelela, Pili Mtambalike, Mwanzo Millinga, Nathan Mpangala na Dkt. Joyce ambaye alikuwa Katibu wa Jopo.
Shughuli ya ugawaji Tuzo hiyo utafanyika jijini Dar es Salaam, siku ya Jumamosi, Aprili 29 katika Hoteli ya Bluepearl na kuhudhuriwa na Mgeni rasmi ambaye ni Mshindi wa Tuzo ya Mafanikio katika Maisha ya Uandishi wa Habari, 2015, Jenerali Ulimwengu.
Friday, April 21, 2017
WANAHABARI 66 KUWANIA TUZO YA UMAHIRI KATIKA UANDISHI WA HABARI 2016
Tags
# HABARI MBALIMBALI
About Unknown
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
HABARI MBALIMBALI
Labels:
HABARI MBALIMBALI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment