Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amekutana na ujumbe kutoka kampuni ya JUMEME inayojishughulisha na uzalishaji wa umeme kwa kutumia nishati ya jua.
Ujumbe huo ulijumuisha baadhi ya wakurugenzi wa kampuni ya JUMEME ambao ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Tanzania (SAUT), Padre Dk. Thadeus Mkamwa na Leo Schiefermueller.
Ujumbe huo ulifika ofisini kwa Waziri Muhongo mjini Dodoma, kumweleza mipango na mikakati yao ya kuendelea na uzalishaji wa umeme wa jua katika maeneo ya Tanzania yaliyo nje ya gridi ya Taifa ya umeme.
Kampuni hiyo, inaendesha mradi wa kuzalisha umeme wa jua katika Kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe na imelenga kuwafikia watu milioni moja ndani ya Tanzania kupitia mitambo 300 katika vijiji vilivyo nje ya gridi ya Taifa ifikapo mwaka 2022.
Profesa Muhongo, kwa upande wake, aliwahakikishia JUMEME kuwa Serikali itawapa ushirikiano unaotakiwa ili kuhakikisha wananchi wa vijijini wanapata umeme kwa kutumia njia mbalimbali muafaka kama ilivyodhamiriwa.
Tuesday, April 11, 2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment