KOCHA
Nabil Maaloul Alhamisi aliteuliwa tena kuiongoza Tunisia kwa mara ya
pili, miaka minne baada ya kufanya kazi hiyo kwa muda wa miezi saba.
Mtu
mzima huyo wa umri wa miaka 54, ambaye aliiongoza klabu ya Esperance ya
Tunisia kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2011, anachukua
nafasi ya Henryk Kasperczak aliyejiuzulu April.
Maaloul alikuwa kocha wa timu ya taifa Februari mwaka 2013, lakini akajiuzulu baadaye mwaka huo.
Kasperczak
aliondoka baada ya Tunisia kutolewa kwenye Robo Fainali za Fainali za
Kombe la Mataifa ya Afrika Januari mwaka huu nchini Gabon.
Taarifa ya Shirikisho la Soka Tunisia (FTF) imesema kwamba uteuzi huo unaanza mara moja.

No comments:
Post a Comment