Shirika la haki za binadamu HRW limesema kuwa Syria imetumia kemikali ya sumu katika mashambulizi mengine matatu ya hivi karibuni.
Shirika la haki za binadamu HRW limesema kuwa Syria imetumia kemikali ya sumu katika mashambulizi mengine matatu ya hivi karibuni.
Hii ni mara ya nne kwa Syria kutumia kemikali hiyo kufanya shambulizi kama ilivyofanya shambulizi Aprili 4 han Sheikhun na kusababisha vifo vya watu takriban mia moja.
Mkurugenzi wa HRW Keneth Roth amesema ni wazi kuwa serikali ya Syria inatumia njia za kinyama katika mashambulizi yake.
Kwa mujibu wa habari,serikali ya Syria imekuwa ikitumia helikopta na ndege za jeshi kupeleka Chlorin na Sarin katika miji ya Damascus,Hama,Idlib na Aleppo.
Ripoti zinaonyesha kuwa mashambulizi ambayo yamekuwa yakifanywa na serikali ya Syria dhidi ya raia wake yanaweza kuwekwa katika kitengo cha uhalifu dhidi ya haki za binadamu.
Shmabulizi la Aprili 4 lilisababisha vifo vya watu wengi wakiwemo watoto thelathini.

No comments:
Post a Comment