Nyani mkubwa albino asiye wa kawaida anatunzwa na kundi moja la kuwalinda wanyama nchini Indonesia baada ya kuokolewa.
Nyani
huyo wa kike mwenye nywele nyeupe na macho ya buluu alikuwa anazuiliwa
katika eneo moja la mashambani nchini Indonesia katika eneo la kisiwa
cha Borneo.
Alikuwa amezuiliwa katika kizimba kidogo kwa siku
mbili na bado alikuwa akionesha tabia za msituni kulingana na kundi hilo
la kuwalinda tumbili la Borneo Orangutan Survival Foundation.
Mnyama huyo huenda akawachiliwa na kwenda msituni ,limesema kundi hilo.
Nyani Albino ni wachache na huyu ni wa kwanza kuchukuliwa na kundi hindi hilo katika historia yake ya miaka 25
Mnyama huyo alikuwa na damu iliokauka katika pua
yake ishara kwamba huenda alipata majeraha alipokuwa akikabiliana na
wanakijiji waliomkamata
Mnyama huyo alikuwa na damu iliokauka katika pua
yake ishara kwamba huenda alipata majeraha alipokuwa akikabiliana na
wanakijiji waliomkamata
Kundi hilo limesema kuwa limebaini kwamba mnyama
huyo alikuwa na tatizo la albino baada ya kumfanyia ukaguzi likisema
kuwa macho yake yalikuwa hayapendi mwanga mwingi.
Mnyama huyo
anayeaminika kuwa na umri wa miaka 5 anachunguzwa katika kituo cha
kubadili tabia cha shirika hilo, ambacho kinawahifadhi zaidi ya tumbili
500.
Tumbili hao wa Borne huorodheshwa kama wanaoangamia na shirika la kitaifa la uhifadhi wa asilia IUCN.
Idadi
yao ilipungua kwa takriban asilimia 60 kati ya 1950 na 2010 kutokana na
uharibifu wa mazingira yao na uwindaji haramu na kushuka zaidi kwa
asilimia 22 kunatarajiwa kati ya 2010 na 2025, kulingana na shirika
hilo.
Mnyama huyo alikuwa na damu iliokauka katika pua yake ishara
kwamba huenda alipata majeraha alipokuwa akikabiliana na wanakijiji
waliomkamata

No comments:
Post a Comment