Kabla ya kukutana na Bw Li, Rais Xi Jinping wa China pia alikutana na mwenzake Kenyatta, na kusema China inapenda kuunganisha mikakati ya maendeleo na Kenya, na kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.
Kwa upande wake Rais Kenyatta amesema, uhusiano kati ya Kenya na China unaendelea kwa kasi na kuzidi kuimarika. Amesema Kenya inapenda kushirikiana na China kudumisha mwelekeo wa mawasiliano ya viongozi, kuhakikisha uhusiano wa pande mbili unaendelea kwa kiwango cha juu, na kuyafanya mafanikio yaliyopatikana katika kutimiza maendeleo na ustawi wa pamoja kati ya nchi hizo mbili yawe mfano wa kuigwa wa ushirikiano wa kunufaishana kati ya Afrika na China.

No comments:
Post a Comment