Bingwa wa ndondi za uzani mzito duniani anayeshikilia taji la WBC Deontay Wilder ameshtakiwa kwa kumiliki bangi.
Maafisa wanasema kuwa walipata dawa hiyo ndani ya gari lake.
Wakili wa Wilder Paul Patterson aliambia kitengo cha habari cha Tuscaloosa kwamba dawa iliopatikana ndani ya gari hilo haikuwa yake na kwamba mtu mwengine alitumia gari hilo wakati bondia huyo alipokuwa safarini.
Alirudi nyumbani leo kutoka Georgia akiwa anaendesha gari lake la Rolls Royce na kuchukua gari jingine aina ya Cadillac Escalade kutembea maeneo mbalimbali ya jimbo hilo.
Wilder alishtakiwa na polisi na kuachiliwa huru kwa dhamana ya dola 1000.
Maafisa walipata ruhusa ya kulisaka gari hilo kabla ya kufanikiwa kupata kiwango cha bangi kutoka kwa gari hilo, taarifa ya maafisa wa polisi wa Tuscaloosa ilisema.
Pigano la mwisho la Wilder lilikuwa la ushindi wa raundi ya tano kwa njia ya Knockout dhidi ya Gerlad Washington alipotetea taji lake la WBC ambalo amemiliki tangu 2015.
BBC Swahili
No comments:
Post a Comment