LATEST NEWS

Friday, June 16, 2017

Jeshi la polisi Wilani Same limeweka kambi katika vijiji vya Heikondi,Rikweni na Tae katika zoezi la kutokomeza zao la Mirungi

Operesheni ya kutokomeza mirungi katika vijiji vya Heikondi, Rikweni na Tae katika Kata ya Tae iliyopo Wilayani Same imeendelea kwa kasi huku jeshi la polisi likisema kuwa halitaacha zoezi hilo.

Kamishina wa Polisi toka mamlaka ya kuthibiti na kupambana na madawa ya kulevya Nchini MIHAYO MSIKHELA,amesema madawa ya kulevya aina ya mirungi yamekuwa yakiwaathiri vikali vijana walio wengi hapa Nchini kitu ambacho amekitaja kuwa kinapoteza nguvu kazi ya Taifa.

Amewahimiza wakazi wa wilaya ya Same kuachana na zao hilo haramu ambalo litawapeleka sehemu mbaya huku akiwataka kujiwekeza katika kilimo cha mazao halali akiyataja mazao ya kahawa,migomba.
Aidha kwaupande wake Mkuu wa Wilaya ya Same Rosemary Staki Senyamule akiongea katika operesheni hiyo amemshukuru Rais wa jamuhuri ya Tanzania DR.John Magufuli kwa kuongeza nguvu katika kupambana na madawa hayo.

Rosemary amesema tokea mwaka jana hadi kufikia hivisasa jumla ya watu 45 wametiwa mbaroni kwa kulima zao hilo haramu huku watu 4 wakiwa wamesha hukumiwa kifungo cha maisha.


No comments:

Post a Comment

Adbox