LATEST NEWS

Tuesday, June 27, 2017

Korea Kaskazini yakataa pendekezo la kushirikiana Olimpiki

Korea Kaskazini imekataa ombi toka Korea Kusini kwamba nchi hizo mbili ziunde timu moja kwa ajili ya michezo ya Olimpiki majira ya baridi mwakani.

Rais mpya wa Korea Kusini Moon Jae-in aliunga mkono ushirikiano huo ambao ulipendekezwa na waziri wa michezo Do Jong-hwan.

Mwananchama wa kamati ya olimpiki ya Korea Kaskazini Chang Un amesema huu si wakati wa kushauriana kuhusu maafikiano. Mataifa hayo mawili yamewahi kushirikiana na kuunda timu moja katika mashindano ya ubingwa wa tenisi ya mezani duniani mwaka 1991

No comments:

Post a Comment

Adbox